Na Baraka Kizuguto, Afrika Kusini
Timu
ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imeendelea na mazoezi katika uwanja
wa Olympia Park kujiandaa na mchezo wa fungua dimba dhidi ya timu ya
Taifa ya Swaziland.
Kocha
mkuu wa timu ya Taifa Stars Mart Nooij amesema vijana wake wanaendelea
vizuri na mazoezi, ikiwa leo ni siku ya pili kufanya mazoezi baada ya
kufanya mazoezi ya kwanza jana jioni.
Nooii
amesema japokuwa kuna hali ya hewa ya baridi katika mji wa Rustenburg,
wachezaji wake wameanza kuizoea na kusema kwa kuwa bado kuna zaidi ya
masaa 72 kabla ya mchezo wa awali watakua wameshaizoea hali ya hewa.
Kuhusu
uwanja wa mazoezi, kocha Nooij amesema hali ya uwanja ni nzuri, uwanja
una nyasi nzuri hali inayopelekea kikosi chake kufanya mazoezi katika
mazingira mazuri.
Akiongelea
mchezo wake wa kwanza wa ufunguzi dhidi ya timu ya Taifa ya Swaziland
utakaochezwa siku ya jumatatu, amesema anawajua Swaziland ni timu nzuri,
mara ya mwisho katika mchezo wa kirafiki walitoka nao sare, hivyo
anawaanda vijana wake kupata ushindi katika mchezo huo.
Kikosi
cha Swaziland kina wachezaji mchanganyiko wakiwemo wanaocheza ligi yao
ya nyumbani na baadhi wanaocheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini.
Taifa
Stars itacheza mchezo wa kwanza dhidi ya Swaziland katika Uwanja wa
Olympia Park siku ya jumatatu saa 1.30 usiku kwa saa za huku, sawa na
saa 2.30 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni