Baada ya kufanya vibaya kwenye mchezo wa nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, Gareth Bale siku zake zinahesabika. Klabu ya Manchester United imeanza kunyemelea baadhi ya mastaa akiwemo Gareth Bale aliye kwenye kuti kavu Real Madrid na pia winga kinda aliye vizuri kwa sasa Harry Kane kwa kuwauza Robin van Persie na Angel Di Maria ambaye anaonekana mpira wa Uingereza umemshinda.
Nao mabingwa Chelsea wanawanyemelea kwa ukaribu wachezaji wa Atletico Madrid Antoine Griezmann, 24, and Koke, 23 kwa gharama zinazoweza kufikia £100m.
Nahodha wa Liverpool ambaye atatimka mwisho mwa msimu akielekea ligi ya Marekani amemuomba winga aliye juu kwa sasa Raheem Sterling asaini mkataba mpya na majogoo hao wa Liverpool. Mchezaji tegemeo wa Manchester City Yaya Toure, 32 anawaniwa na Inter Milan ya Italia.Kiungo wa Kaizer Chiefs Siyabonga Nkosi anawaniwa na vilabu vitatu ambavyo ni Free State Stars, Mpumalanga Black Aces na Platinum Stars.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni