WACHEZAJI wanne wa klabu
ya River Plate wamekimbizwa hospitali baada ya kupuliziwa pilipili na
mashabiki wa Boca Juniors hatua ilipelekea mchezo wao wa Copa
Libertadores kuahirishwa.
Mchezo huo wa maruadiano hatua ya mtoano
uliofanyika Buenos Aires, Argentina, ulisimamishwa wakati timu hizo
zikiwa hazijafunga baada ya wachezaji kushambuliwa wakati wakitoka
katika vyumba vyao wakati wa mapumziko.
Tukio hilo limelaaniwa vikali
napande zote mbili huku rais wa Boca Juniors Daniel Angelici akidai kuwa
watafanya kila wawezalo kushirikiana na polisi ili kuwanasa wahalifu
hao.
Picha za video zilizokuwa zikiwaonyesha wachezaji wa River Plate
Leonardo Ponzio na Leonel Vangioni wakisugua macho yao huku wachezaji
wengine wakinawa maji usoni baada ya kupuliziwa pilipili.
Baadhi ya
wachezaji walisikika wakilalama kuwa hawaoni huku macho yao yakiwaka
moto hatua ilipelekea mwamuzi kusitisha pambano hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni