MENEJA wa Arsenal,
Arsene Wenger amekiri kuingiwa na wasiwasi kuwa mahasimu wao wa Ligi Kuu
Manchester United watatumia fedha walizonazo kuwanasa wachezaji
anaowawinda kuwasajili katika majira ya kiangazi.
United ambao tayari
imetangaza kumsajili winga wa PSV Eindhoven Memphis Depay kea kitita cha
euro milioni 27.5, itatumia fedha nyingi katika usajili huu kama
walivyofanya mwaka jana wakati walimpowanunua kina Angel Di Maria, Ander
Herrera, Luke Shaw, Marcos Rojo na Daley Blind wakitumia karibu euro
milioni 200.
Wenger anaamini meneja wa United Louis van Gaal atatumia
kiasi kama hicho cha fedha katika usajili wa kiangazi hiki. Akihojiwa
Wenger amesema anategemea United kuwa tishio katika kipindi cha usajili
kwani kila mchezaji anayemuwania wapinzani wao hao nao wanakuwa
wanamtaka.
Arsenal itasafiri kuelekea Old Trafford kupambana na
Manchester United Jumapili hii.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni