KLABU ya Arsenal, imeripotiwa kupanga muda wao kwa ajili ya kutangaza usajili wa nyota wa Juventus, Arturo Vidal.
Vidal alikuwa katika mipango ya usajili ya Manchester United kiangazi mwaka jana lakini walikatishwa tamaa kufuatia Juventus kutaka kitita cha paundi milioni 40.
Hata hivyo, kutokana na taarifa zilizotolewa hivi karibuni nchini Italia, Liverpool wameambiwa kuwa wanaweza kumsajili nyota huyo wa kimataifa wa Chile kwa paundi milioni 25.
Taarifa hizo zinachanganya zaidi baada ya mwandishi wa habari kutoka Argentina Hernan Feler sasa kudai usajili wa Vidal kwenda Arsenal umeshakamilika.
Mwandishi huyo ambaye anaripotiwa kuwa ndiye aliyevujisha taarifa za Arsenal kutaka kumsajili Alexis Sanchez kutoka Barcelona msimu uliopita, aliandika katika ukurasa wake wa twitter kuwa baada ya michuano ya Copa America klabu itatangaza rasmi kumsajili nyota huo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni