MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amesema nahodha wake, Mikel Arteta ambaye hajacheza toka Novemba mwaka jana kwasababu ya majeruhi anaweza kuwa fiti kwa ajili ya mchezo wa fainali ya Kombe la FA dhidi ya Aston Villa utakaofanyika Jumamosi hii.
Akihojiwa Wenger amesema uwezekano wa kumtumia Arteta katika mchezo huo ni mkubwa kwasababu yuko fiti na amekuwa akifanya mazoezi na wenzake.
Kocha huyo aliongeza kuwa beki wa kimataifa wa Ufaransa Mathieu Debuchy pia ana nafasi ya kuwepo katika kikosi chake lakini mshambuliaji wa kimataifa wa Uingereza Danny Welbeck hatakuwa fiti kwa ajili ya mchezo huo.
Wenger pia amepata ahueni baada ya nyota wake Jack Wilshere na Theo Walcott kuonyesha kurejesha makali yao kwa kucheza kwa kiwango cha juu katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu dhidi ya West Bromwich Albion ambao walishinda mabao 4-1.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni