MENEJA wa Liverpool, Brendan Rodgers amekubali kuwa kibarua chake kiko mashakani baada ya mchezo wa mwisho wa nahodha Steven Gerrard kumalizika kwa kipigo kizito.
Liverpool ilimuaga nahodha wake huyo kwa kukubali kipigo cha mabao 6-1 dhidi ya Stoke City na kuwafanya kumaliza nafasi ya sita katika msimamo wa Ligi Kuu.
Akihojiwa Rodgers ambaye ameshinda michezo miwili katika ya tisa aliyoisimamia Liverpool hivi karibuni, amesema yuko tayari kuondoka kama wamiliki wakimtaka kufanya hivyo.
Kocha huyo aliendelea kwa kuomba radhi kwa kipigo hicho kizito walichopata ingawa amedai bado kuna mengi mazuri anayoweza kuifanyia klabu hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni