KLABU ya Liverpool iko tayari kumtoa Rickie Lambert ili waweze kumsajili Christian Benteke kutoka Aston Villa.
Mshambuliaji huyo ni mmoja kati ya nyota waliopo katika mipango ya usajili ya Liverpool majira haya ya kiangazi na wanaweza kuchuana na Chelsea kuwania saini yake.
Hata hivyo Liverpool wanafahamu kuwa Villa walikuwa wakimtaka Lamberty Januari na wanawea kuwa tayari kumuofa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uingereza ili waweze kumpata Benteke.
Lambert mwenye umri wa miaka 33 aliamua kubakia Januari na kupigania nafasi yake Anfield lakini Villa, Crystal Palace na Bournemouth wote wameonyesha nia ya wazi kutaka kumsajili kiangazi hiki.
Liverpool wamepania kufanya usajili mkubwa kiangazi hiki huku nyota kama James Milner na danny Ings wote wakitegemewa kutua Anfield.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni