Kocha
wa Arsenal Arsene Wenger ameonyesha kusikitishwa na vijana wake kwa
kukosa makali mbele ya goli katika mchezo dhidi ya Sunderland uliopigwa
jana usiku katika uwanja wa Emirates, ambapo timu hizo zilitoka suluhu.
Hii
ni mechi ya tatu ambapo Arsenal wameshindwa kupata ushindi katika
uwanja wao wa nyumbani, baada ya ile ya Chelsea, Swansea na hii ya
Sunderland.
"Tunaweza
kusema kuwa tuliutawala mchezo kwa kiasi kikubwa sana lakini kwa sasa
tunakosa yale makali na jinsi ya kuzitumia nafasi katika safu yetu ya
ushambuliaji,"Wenger aliwaambia waandishi.
"Tulikuwa
wachovu kidogo usiku wa jana. Pia hatujafunga ndani ya michezo mitatu
tuliyocheza nyumbani na hiyo pengine ni sababu kubwa sana ya sisi kukosa
kujiamini.
"Lakini
hata hivyo ni lazima utarajie mpinzani wako kucheza vizuri. Tuko katika
nafasi nzuri ya kumaliza katika nafasi tatu za juu. Hivyo ngoja
tufanikishe hilo.
"Hatukuonekana
kama tungepata goli, Kiukweli. Hata kama tulipiga mashuti 20 golini,
lakini mara zote kulikuwa kuna kitu kinakosekana. Tulihitaji kitu fulani
maalum ili tuweze kupata goli kutokana na ukweli kwaba walilinda kwa
umakini wa hali ya juu. Mara zote kulikuwa na kizuizi pale hasa
[Sebastian] Coates na [John] O’Shea katika mipira ya krosi.
"Pointi
moja tuliyoipata kutoka kwa Man United Jumapili ilikuwa ni muhimu sana.
Kama tungeikosa ile tungekuwa na hatari kubwa sanae."
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni