Pamoja
na kuwepo kwa taarifa za kuondoka kwake kwenda Real Madrid, kipa David De Gea
ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Manchester United.
De
Gea ameshinda tuzo hiyo kutokana na umahiri aliouonyesha msimu huu ambao timu
yake imebakiza mechi moja.
Man United sasa angalau ina uhakika wa kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya na
kipa huyo alikuwa mwokozi katika mechi nyingi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni