Mshambuliaji
wa Liverpool Raheem Sterling alizomewa na mashabiki wa klabu hiyo
wakati wa utoaji wa tuzo mbalimbali za msimu kwa wachezaji wa timu hiyo.
Sababu
kubwa ya kinda huyo raia wa Uingereza kuzomewa ni kutokana na msimamo
wake wa kutaka kuondoka klabuni hapo mara baada ya kukataa ofa ya mpya
ya mshahara wa paundi 100,000 kwa wiki hali ambayo imewaudhi sana
mashabiki wa Liverpool.
Sterling alichaguliwa kuwa mchezaji bora kijana wa msimu huu kwa klabu ya Liverpool.
Raheem
Sterling alichaguliwa kuwa mchezaji bora kijana wa msimu huu wa klabu
ya Liverpool katika sherehe iliyofanyika huko Echo Arena jana Jumanne.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni