NAHODHA Liverpool
anayeondoka, Steven Gerrard anatarajiwa kucheza mechi yake ya kwanza
akiwa na klabu yake mpya ya Los Angeles Galaxy Julai 11 mwaka
huu.
Kiungo huyo mkongwe mwenye umri wa miaka 34, anatarajia kuwepo
katika mchezo wa nyumbani dhidi ya klabu ya America ya Mexico michuano
ya Kombe la Kimataifa.
Ofisa mkuu wa Galaxy, Bruce Arena wanategemea
Gerrard kuwepo kabla ya Julai 11 kwa ajili ya kufanya mazoezi na wenzake
kwa ajili ya mchezo huo.
Kwasasa Gerrard yuko katika mapumziko ya msimu
na wachezaji wenzake wa Liverpool, Dubai lakini anatarajiwa kuelekea
nchini Marekani kuanza changamoto mpya na anatarajiwa kuwa mchezaji
rasmi wa Galaxy kuanzia Julai 8 mwaka huu.
Gerrard ameasaini mkataba wa
miaka miwili na klabu hiyo baada ya kutangaza Januari kuwa ataondoka
Liverpool klabu ambayo ameitumikiakwa miaka 17.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni