Mourinho amekiri kuwa itakuwa vigumu kukiimarisha kikosi chake hicho zaidi ya kilivyo hivi sasa.
Chelsea walitawadhwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu msimu wa 2014-2015 huku wakiwa wamebakisha michezo mitatu mkononi.
Akihojiwa Mourinho anataka kutetea taji lake hilo msimu ujao lakini hadhani kama wachezaji wapya watamsaidia kufanikisha adhma yake hiyo kulinganisha na alionao sasa katika kikosi chake.
Mabingwa hao hivi sasa wako Bangkok, Thailand kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya wachezaji nyota wa Ligi Kuu ya nchi hiyo utakaofanyika katika Uwanja wa Rajamangala, Jumamosi hii
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni