Kocha Goran Kopunovic aliyepewa mkono wa Kwaheri Msimbazi |
Milovan anayetarajiwa kurudi Msimbazi |
Kocha Piet de Mol wa Ubelgiji anayetajwa kuja kuchukua mikoba ya Goran ndani ya Simba |
Hata hivyo uongozi huo tayari umeanza mchakato wa kusaka kocha mkuu mpya na tayari makocha sita toka nchi za Ujerumani, Ufaransa, Bulgaria, Serbia, Ubelgiji na Croatia wametuma maombi yao na uongozi wa Simba utaanza mchakato wa kupitia wasifu wa makocha hao kabla ya kumchukua mmoja.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zakaria Hanspope akiwa safari nje ya nchi alizungumza na chombo kimoja cha habari kuwa, wameshindwana na Goran na sasa wanafanya taratibu za kumsaka kocha mpya ambaye atatangazwa mapema baada ya kupitiwa kwa wasifu wa makocha waliotuma maombi.
Hanspope alisema kuna orodha ya majina sita ya makocha toka barani Ulaya walioomba nafasi ya kumrithi Goran na utafanyika mchujo kabla ya kutoa jina moja la kubeba majukumu ya kuinoa Simba mpya kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
"Niko safarini, lakini taarifa nilizonazo ni kwamba tumeshindwana na Goran na tunasaka kocha mpya na tayari kuna majina sita yameshawasilisha maombi yao, kutoka nchi za Ubelgiji, Ufaransa, Serbia, Bulgaria na yatapitiwa wasifu wao na atakeyeenda na sifa ya klabu yetu tutamchukua," alisema Mwenyekiti huyo na kusisitiza kuwa ilikuwa ngumu kukubaliana na Goran juu ya masilahi.
"Goran alitaka masilahi makubwa ambayo klabu imeona isingeweza na tulimpa nafasi ya kujifikiria, lakini hata hivyo bado msimamo wake ulikuwa haujatulainisha kuafikiana naye, hivyo tumeachana naye na sasa tunaangalia mambo mengine," alisema.
Ingawa Hanspope alishindwa kutaja majina ya makocha hao walioomba kazi, lakini mmoja ya wanaotajwa kuwa na nafasi kubwa ya kumrithi Kopunovic ni Piet de Mol kutoka Ubelgiji ambaye ana rekodi na uzoefu wa soka la Afrika, huku Cirkovic Milovan akielezwa kuwa naye yu tayari kurudishwa katika kikosi hicho, huku akibebwa na rekodi zake kwa timu hiyo.
Juu ya usajili, zakaria Hanspope alisema ni mapema kwa sasa kwa sababu wanasubiri kwanza wapate kocha mpya ambaye atakuwa na mapendekezo yake, ingawa wameshaanza kuwasainisha wachezaji wao wa kikosi cha msimu ulioisha hivi karibuni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni