Nyota wa Chelsea Eden Hazard amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa chama cha waandishi wa habari za michezon nchini Uingereza huku mshambuaji hodari kinda wa Tottenham Harry Kane akishikilia nafasi ya pili na John Terry akishika nafasi ya tatu.
We're pleased to announce that @ChelseaFC's Eden Hazard is this year's FWA Footballer of the Year! Congratulations @hazardeden10 #cfc #epl
Hazard,
ambaye alichukua pia tuzo ya mchezaji bora wa mwaka ligi kuu Uingereza
(PFA Player of the Year award) mwezi uliopita, amepata karibuni asilimia
53 ya kura zote za vyombo vya habari nchini, huku akiwa ni chachu kubwa
sana kwa timu yake kutwaa ubingwa wa EPL msimu huu tangu walipochukua
mara ya mwisho mwaka 2010.
Akiwa
pamoja na John Terry na Branislav Ivanovic, Mbelgiji huyo ni miongoni
mwa wachezaji pekee wa Chelsea ya Mourinho ambao walianza kila mchezo
msimu huu, akifunga mabao 14 na kutoa pasi za magoli 14.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni