STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatano, 27 Mei 2015

KILICHOJIRI LEO KUHUSU KESI YA JUMA KASEJA, JAJA NA YANGA...


'Kaseja aliwahi kuwa kipa namba moja Tanzania aking'ara na kikosi cha Simba.'

KESI inayomkabili kipa mkongwe Juma Kaseja Juma dhidi ya Yanga, imeshindwa kumalizika leo baada ya Mahakama ya Kazi - Kitengo cha Uamuzi kuipiga kalenda kwa mara nyingine.

Uongozi wa Yanga umemfungulia mashtaka kipa huyo wa zamani wa Simba kwa madai ya kukiuka masharti ya mkataba kati yake na klabu hiyo ya Jangwani alipoamua kuikacha baada ya kupishana kauli na uongozi.

Kaseja alidai kutolipwa kwa wakati mwafaka sehemu ya fedha za ada za usajili wake kwa mabingwa hao mara 25 wa Tanzania Bara.

Katika kesi hiyo leo, Mahakama ya Kazi imeshindwa kutoa uamuzi kutokana na wakili wa Kaseja, Samson Mbamba kutofika mahakamani.

Yanga iliwakilishwa na mwanasheria wake, Frank Chacha, huku wakili wa Kaseja akituma mwakilishi ambaye aliiomba mahakama kuahirisha shauri hilo kwa kuwa Mbamba alikuwa na shauri jingine kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania.

Mahakama ilipokea ombi hilo na kuipika kalenda kesi hiyo ya madai hadi Juni 26, mwaka huu.

JAJA NAYE HAJATOKEA
Kuhusu kesi inayomkabili mshambuliaji Geilson Santos Santana 'Jaja' dhidi ya Yanga, mahakama pia imeipiga kalenda kesi hiyo kutokana na upande wa mlalamikiwa (Jaja) kutowafika mahakamani.

Endapo Jaja hatatokea mahakamani mara tatu, kesi italazimika kusikilizwa upande mmoja na kutolewa uamuzi.
CHANZO; MPENJA

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox