STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatano, 27 Mei 2015

MUENDELEZO KUELEKEA FAINALI YA UEFA

MR'CHOI na PAUL MALDIN Kama kawa tunazidi kulisongesha na mkongwe Maldin maana tusha pumzika vya kutosha ngoja safari iendelee Ila tambua Paul Cesare Maldin ni mzaliwa wa Milan tarehe 26/6/ 1968 maisha yake yote ya soka kakipiga Ac Milan akiwa kama beki wa kushoto na kati.
Alianza kukipiga Ac milan 1978 katika timu ya vijana wakati huo Liverpool walikuwa wamechukua ubingwa wao wa pili wa Uefa wakati mwaka alio zaliwa 1968 Manchester United walikuwa wanachukua ubingwa wao wa kwanza na amedumu kwa miaka 25 viunga vya milan. Maldin- Poa nadhani panatosha turudi kwenye njia kuu ya safari yetu jana tuliangazia mabingwa ngoja tuangazie upande wa magoli. Choi- Hapo sawa maana utamu upo kotekote wajua ni hadimu sana kuangazia vitu kama hivi katika mabara mengine hususani yale yanayo ibukia kwa sasa kwenye soka. Maldin- Mtu wa kwanza kutikisa nyavu alikuwa ni João Baptista Martins aliekuwa anakipiga Sporting Cp katika mchezo dhidi ya Partizan tarehe 4/9/1955 ambapo fainal zake za kwanza zilifanyika Parc Des Princes kati ya Reims na Real Madrid. Choi- Du noma sana kwa kiungo huyo wa Ureno mzaliwa wa Sines 3/9/1927 alie kidumu Sporting Cp kwanzia 1947-1959 jamaa aliandika historia isiyo sahulika na kama unakumbuka alifariki 18/11/1993 kipindi ambacho kulianza muonekano mpya wa Uefa. Maldin- Alfredo Di Stephano wa Real Madrid zama zile ndo alikuwa kinara wa mabao kwenye michuano hii alikuwa na magoli 49 katika michezo 58 kwanzia 1955-1964 huku mkongwe mwenzake Eusebio wa Ureno alikuwa na magoli 46 akikipiga kwanzia 1961-1974 pale Benfica. Maldin- Katika orodha ya wachezaji kumi wenye magoli mengi hao ndo wakongwe pekee waliopo kinara ni Messi alie anzia kukipiga 2005 akifuatiwa na C.Ronaldo nae ana 77 alieanzia kukipiga 2003 na ndo wachezaji pekee waliopo katika orodha ya kumi bora wanao endelea kukipiga katika mashindano haya. Choi- Pia Maldin kumbuka kwenye hiyo orodha anae shika nafasi ya 10 ni mwana wa Tembo kule Magharibi mwa Afrika Didier Drogba wa Ivory Cost akiwa na magoli 44 mchezaji pekee wa Afrika mwenye idadi kubwa ya magoli ndani ya Uefa. Maldin-Sawa pia kwenye hiyo orodha wapo kina Raul 71,Van Nistelrooy 56,Henry 50, Shevshenko 48 na Inzaghi 46 kwa maana hiyo muonekano mpya wa Uefa ulio anza 1992 ndo umetoa idadi kubwa ya magoli . Choi- sawa tuongeze spidi tuwa angazie wahusika ila jua katika msimu mpya wa Uefa Juul Ellerman alie kuwa anakipiga Psv-Eindhoven ndie mchezaji wa kwanza kufunga magoli matatu kwenye mchezo mmoja ilikuwa 16/9/1992 dhidi ya Fk Zalgiris Vilnius. Maldin- bado twazidi kusonga tambua mchezaji aliefunga magoli matatu katika umri mdogo alikuwa Raul Gonzalez '18', pia hapo kuna jumla ya wachezaji 76 waliofunga magoli matatu katika mchezo mmoja kutoka mataifa 32 ila ni wachezaji 11 pekee waliofanikiwa kuvuka zaidi ya magoli matatu na wachezaji wawili tu waliofikisha magoli zaidi ya manne. Choi- hapo zaidi ya matatu ni Marco van Basten,Inzaghi,Dado Piso,Van Nistelrooy,Shevshenko, Bafetimbi Gomis, Mario Gomez, Lewandowski,Ibrahimovich, Adriano na Messi. Zaidi ya manne nazungumzia magoli matano ni Lionel Messi na Luiz Adriano. Maldin- Kituo cha pili tupumzike maana dah! ila kupitia hizo takwimu utangua si lazima ucheze timu kubwa ndo uweke rekodi juhudi hufanywa muda wowote katika mazingira yote. MAONI:: Choikangta.ckt@gmail.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox