STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 28 Mei 2015

SEVILLA WATWAA 'NDOO' YA EUROPA... ANGALIA PICHA ZA SHANGWE

Wachezaji wa Sevilla wakishangilia baada ya kipyenga cha mwisho.

HATIMAYE Sevilla wameibuka mabingwa wa ligi ya Europa baada ya kupata ushindi wa magoli 3-2 dhidi ya Dnipro katika mechi ya fainali iliyomalizika usiku huu National Stadium, Warsaw.
Mapema dakika ya 7' Dnipro waliandika bao la kuongoza kupitia kwa Nikola Kalinic, lakini dakika ya 28' Grzegorz Krychowiak akaisawazishia Sevilla.
Dakika ya 31' Carlos Bacca akaifungia Sevilla goli la pili, lakini Ruslan Rotan akaisawazishia Dnipro dakika ya 44'.
Carlos Bacca ndiye aliyeibuka shujaa baada ya kufunga goli la tatu na la ushindi kwa Sevilla katika dakika ya 73'.
Sevilla kwa mara nyingine tena wamechukua ubingwa wa EUROPA baada ya kuwatungua Dnipro kwa mabao 3-2 na kuwa klabu ya kwanza barani Ulaya kushinda taji hilo mara nne kwa matokeo yanayofanana yaani magoli 3-2 mara hizo zote. 
Wahispania hao mara ya kwanza walichukua miaka ya 2006 and 2007 wakati huo likiitwa Uefa Cup - na sasa wamechukua tena kwa mara ya pili mfululizo huku Carlos Bacca akipiga mbili na kujihakikishia ushujaa wa mchezo.
Wababe hao wa Unai Emery mwaka jana walishinda kwa mikwaju ya penati baada ya mchezo kumalizika kwa are ya  0-0 dhidi ya Benfica, lakini wakati huu wamekataa kabisa kufika huko.
Grzegorz Krychowiak aliipatia Sevilla bao la kwanza huku Bacca akiongeza la pili na tatu na kuhitimisha ushindi kwa wababe hao wa EUROPA.
Nao Dnipro ambao wanatokea nchini Ukraine walijipatia magoli yao kupitia kwa nahodha wao Ruslan Rotan na Nikola Kalinic.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox