Simba imefanikiwa kumnasa beki wa kushoto wa Azam FC, Samir Hajji Nuhu na kumsainisha mkataba jijini Dar es Salaam, jana usiku.
Beki huyo amesaini mkataba wa kuichezea Simba kwa mwaka mmoja.
Beki huyo aliyewahi kuichezea Taifa Stars amesaini mkataba huo mbele ya mjumbe wa kamati ya usajili ya Simba, Collins
Frisch.
Uongozi wa Simba umeonyesha umepania kuimarisha safu yake ya ulinzi baada ya kumnasa beki wa JKT, Mohammed Fakhi, jana usiku.
Faki amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Simba jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amethibitisha.
“Kweli Faki amesaini miaka miwili, hii ni sehemu ya kuhakikisha tunaimarisha safu ya ulinzi,” Hans Poppe alikaririwa na Salehjembe.
Faki aliichezea JKT kwa ufanisi mkubwa katika msimu uliopita.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni