TAARIFA
mpya leo zinasema kocha mkuu wa Simba aliyemaliza mkataba wake, Mserbia
Goran Kopunovic amekubali kurejea Dar es salaam kuendelea na kazi ya
kuwanoa vijana wa Msimbazi wenye uchu wa mafanikio kuelekea msimu mpya
wa ligi kuu soka Tanzania bara.
Tayari
Simba kupitia kwa mwenyekiti wa kamati ya usajili, Zacharia Hans Poppe
walithibitisha kuachana na Kopunovic kwasababu ya kutaka dau kubwa la
usajili na mashahara mrefu, hivyo kuanza harakati za kusaka kocha mpya.
Kopunovic
alitakiwa kutoa jibu kufikia Ijumaa ya wiki iliyopita kama atasaini
mkataba mpya au la!, lakini alishindwa kufanya hivyo.
Kopunovic
alitaka dola za Kimarekani 50,000 (sawa na Sh. Milioni 100) kama dau la
kusaini Mkataba na mshahara wa dola 8,000 (Sh. Milioni 16) kwa mwezi,
kiasi ambacho Simba walisema hawawezi kulipa.
Sasa
Mserbia huyo amekubali kushuka dau na atarejea nchini kuanzia juma
lijalo kusaini Mkataba mpya na mara moja kuanza maandalizi ya michuano
ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.
Yuke
kocha Mbelgiji Piet de Mol aliyeripotiwa kuja kesho kuwania nafasi ya
Kopunovic, atakuja kama kawaida, lakini kutafuta kazi klabu nyingine.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni