Manchester
United wameitaka Real Madrid kulipa dau la usajili la paundi milioni 29 kama
wanaitaka saini ya mlinda mlango David De Gea anayeripotiwa kufikia makubaliano
binafsi na miamba hiyo ya Hispania.
De Gea
amebakiza miezi kumi na minne katika mkataba wake wa sasa na dalili zote za
kutimka Old Trafford zimeonekana, lakini Manchester United na Real Madrid bado
hazijakubaliana ada ya usajili ya kipa huyo mwenye miaka 24.
Vyombo
vya habari vya Hispania vinadai kuwa United wanahitaja euro milioni 40 sawa na
paundi milioni 28.6 ili kumuachia kipa huyo wa kimataifa wa Hispania, lakini
Real wanataka kumuhusisha katika usajili huo mlinzi wao, Fabio Coentrao.
Mbali na
hayo, Man United pia inahusishwa na mpango wa kumsajili nyota wa Real Madrid,
Gareth Bale na habari zilizotoka Hispania leo zinaeleza kuwa winga huyo hatajumuishwa
katika usajili wa De Gea.
Wakati
huo huo ripoti zinasema kuwa De Gea atatuta Bernabeu hata kama mlinda mlango
chaguo la kwanza kwa sasa, Iker Casillas ataendelea kuwepo au hapana.
Hatima ya Casillas katika mji wa Madrid ipo shakani kutokana na kushuka kwa kiwango chake na kusababisha agombanie nafasi ya kuanza na Keylor Navas
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni