SHIRIKISHO la soka la
Ulaya-UEFA linajiandaa kulegeza sheria ya mwaka 2011 inayozuia vilabu
vya bara hilo kufanya matumizi ya ziada.
Katika mahojiano na redio ya
Ufaransa RTL, rais wa UEFA Michel Platini amesema kuwa sheria hiyo
ilikuwa ikifanya kazi vizuri lakini itaboreshwa zaidi mwishoni mwa msimu
huu.
Hatua hiyo inafuatia ripoti katika gazeti la Le Parisien siku ya
jumapili iliyosema kuwa kuna mabadiliko muhimu yatakayofanywa katika
sheria hiyo.
Manchester City, Barcelona na Paris Saint-Germain wamekuwa
wahanga wa kwanza wa sheria hiyo baada ya kupigwa faini na adhabu mwaka
jana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni