ZAIDI wa watu 50
wamekamatwa na wengine kuwekwa chini ya upelelezi ikiwa in matokeo ya
uchunguzi wa tuhuma za upangaji matokeo katika mechi za soka nchini
Italia.
Waendesha mashitaka wanaopambana na kundi haramu la Mafia katika
mji wa Catanzaro uliopo kusini mwa Italia ndio walioongoza uchunguzi
huo ambao umepeleka kukamatwa kwa watu hao.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka
vyombo vya habari vya Italia, waliokamatwa in wachezaji 15, marais sita
wa vilabu, maofisa nane wa michezo, makocha na viongozi 10 wa taasisi
za kamari nchini humo.
Uchunguzi huo uliohusisha polisi ilifanyika kwa
kuzifuatilia mechi za ligi daraja la tatu, nne na tano ambazo ndio
zimekuwa zikiongoza kwa tuhuma za upangaji matokeo.
Mpango huo wa kupiga
vita upangaji matokeo ni mkakati wa kuliokoa soka la nchi hiyo ambalo
lilikuwa limegubikwa na vitendo hivyo kuanzia timu za daraja la juu
mpaka chini.
Mwaka 2006 mabingwa wa sasa wa Serie A Juventus walishushwa
daraja huku timu zingine zikikatwa alama baada ya kukutwa na hatia ya
kuhonga waamuzi ili wawape upendeleo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni