Mane alifunga magoli hayo katika dakika ya 13' 14' na 16 hivyo kuvunja rekodi ya hat trick iliyokuwa inashikiliwa na mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Robbie Fowler aliyefunga mabao matatu ndani ya dakika tano.
Rekodi hiyo ya Fowler imeendelea kudumu kwa kipindi cha zaidi ya miaka nane (8).
Magoli
mengine ya Southampton anayochezea mshambuliaji wa kimataifa wa Kenya,
Victor Wanyama yamefungwa na Shane Long katika dakika ya 26' na 38' na
Graziano Pelle alifunga goli la sita dakika ya 81.
Christiani Benteke aliifungia Aston Villa goli la kufutia machozi katika dakika ya 45'.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni