STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 14 Mei 2015

TAIFA STARS YATUA RUSTENBURG , WABONGO WAJITOKEZA KUILAKI!

Baadhi ya Wachezaji wa Taifa Stars baada ya kuwasili Afrika kusini

TIMU ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imewasili leo mchana majira ya saa 6 kamili katika jiji la Rustenburg na kufikia katika hoteli ya Hunters Rest - Protea iliyoypo pembeni kidogo ya  jiji.

Taifa Stars ambayo iliondoka jana joni jijini Dar es salaam jijini Dar es salaam na kufika OR Tambo saa 5 usiku, ilipata mapokezi mazuri kutoka kwa waandaji wa michuano ya COSAFA pamoja na watanzania wanaoishi jijini humo, ililala katika hoteli ya Southern Sun.

Safari ya kutoka Johannesburg kuelekea Rustenburg ilichukua takribani masaa mawili na msafara wa Taifa Stars unaongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF Ephaphra Swai.
Baadhi ya Watanzania waishio Afrika kusini walijitokeza uwanja wa Ndege kuipokea Taifa Stars

Wachezaji waliopo na timu Rutsenburg ni Deogratius Munish, Mwadini Ali, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Oscar Joshua, Haji Mwinyi, Salim Mbonde, Aggrey Moriss, Joram Mgeveke, Said Juma, Hassan Dilunga, Said Ndemla, Abdi Banda, Mwinyi Kazimoto, Ibhrami Ajib, Juma Luizio, John Bocco, Mrisho Ngasa na Saimon Msuva.

Kikosi cha Taifa Stars kinatarajiwa kufanya mazoezi leo jioni katika uwanja wa Rustenburg Impala Bowling Club majira ya saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Kusini sawa na saa 11 jioni kwa Afrika Mashariki.
Watanzania walijitokeza kuipokea Taifa Stars

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox