SARE
ya 1-1 waliyopata Real Madrid kipindi cha pili jana usiku Santiago
Bernabeu inaweza kuhitimisha safari ya soka ya Iker Casillas.
Casillas, aliye kwenye kiwango kizuri msimu huu aliokoa michomo ya hatari iliyopigwa na Claudio Marchisio na Paul Pogba.
Juventus walifunga goli la kusawazisha kipindi cha pili kupitia kwa Alvaro Morata.
Mlinda
mlango gwiji wa Hispania pia aliungana na wachezaji wenzake
kushambulia, lakini dakika ya 93 alizua kituko baada ya kupata mpira wa
kurusha.
Casillas alichukua mpira haraka na kutaka kumrushia Marcelo, lakini alisahau sheria za mpira wa miguu katika urushaji wa mpira.
Mpira
haukuvuka kichwa cha Casillas na mwamuzi Jonas Eriksson akaamuru iwe
adhabu na Juventus wakapewa nafasi ya kurusha baada ya kipa huyo
kuchemsha.
Na
hapo ndipo ndoto za Real Madrid zikazima na kama Iker Casillas
angefanikiwa kusababisha goli ingekuwa historia kubwa katika maisha yake
ya soka.
Kama
kawaida, Internet imefanya kazi yake kama wengi walivyotarajia ambapo
watu wametengeneza picha kumkejeli Casillas....Angalia picha chini
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni