MSIMU wa soka nchini
Hispania umeruhusiwa kumalizika baada ya tishio la kusimamishwa
lililotolewa na Shirikisho la Soka la Hispania-RFEF na mgomo wa
wachezaji kusogezwa mbele na mahakama ya taifa nchini humo.
RFEF
walikuwa wakitaka kusimamisha mechi za mwisho wa msimu zilizobakia na
umoja wa wachezaji uliamua kuitisha mgomo kutokana na sakata la haki za
matangazo.
Barcelona wataweza kushinda taji la La Liga Jumapili hii huku
wakiwa wamebakia na mchezo mmoja kama wakifanikiwa kuwachapa mabingwa
watetezi Atletico Madrid.
Fainali ya Kombe la Mfalme ambayo pia
itawakutanisha na Barcelona na Athletic Bilbao itaendelea kama
ilivyopangwa Mei 30 mwaka huu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni