NAHODHA wa Liverpool,
Steven Gerrard ambaye anaondoka mwishoni mwa msimu huu, amesema anajuta
kutoshinda taji la Ligi Kuu katika kipindi chote alichoitumikia klabu
hiyo.
Gerrard mwenye umri wa miaka 34 anatarajiwa kucheza mchezo wake wa
mwisho Anfield, Jumamosi hii dhidi ya Crystal Palace kabla ya
hajajiunga na Los Angeles Galaxy ya Marekani mwezi ujao.
Akihojiwa
Gerrard amesema angefurahi zaidi kuondoka Liverpool akiwa na medali ya
Ligi Kuu lakini hilo halitawezekana na ndio kitu kikubwa anachojutia
kukikosa katika maisha yake ya soka Anfield. Gerrard anaondoka Liverpool
akiwa ameichezea mechi zaidi ya 700 katika misimu 17 ambayo amekuwa
nao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni