SHIRIKA la misaada la
Save the Children limekanusha taarifa kuwa Cristiano Ronaldo ametoa
msaada ya euro milioni saba kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi
nchini Nepal.
Kauli ya shirika hilo imekuja kufuatia taarifa kuwa
Ronaldo mwenye umri wa miaka 30 ametoa kiasi hicho cha fedha kwenda
kusaidia waathirika wa tetemeko hilo.
Katika taarifa ya shirika hilo
iliyotolewa leo imedai kuwa kuwa Ronaldo akiwa balozi wao amekuwa
akipaza sauti kueleza matatizo wanayokutana nayo watoto duniani.
Lakini
taarifa hiyo iliendelea kudai kuwa ripoti za hivi karibuni kuwa Ronaldo
ametoa fedha kwa shirika hilo la Save the Children kwa ajili ya
waathirika wa Nepal sio za kweli.
Zaidi wa watu 8,000 walifariki dunia
katika tetemeko kubwa lililoikumba nchi hiyo Aprili 25 mwaka huu kabla ya
lingine kutokea Mei 12 na kuuwa wengine 16.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni