Madrid walishindwa kupinduka matokeo ya kufungwa mabao 2-1 katika mchezo wa mkondo wa kwanza dhidi ya Juventus baada ya kujikuta wakipata sare ya bao 1-1 na kuwafanya mabingwa hao wa Serie A kusonga mbele kwa jumla ya mabao 3-2.
Akihojiwa mara baada ya mchezo huo, Ancelotti amesema ni mapema mno kuzungumzia mustakabali wake kwani bado msimu haijamalizika.
Juventus inatarajia kupambana na Barcelona katika mchezo wa fainali utakaofanyika Juni 6 mwaka huu katika Uwanja wa Olimpiki jijini Berlin, Ujerumani.
Mara ya mwisho Juventus kutinga fainali ya michuano hiyo ilikuwa mwaka 2003 wakati walipofungwa na AC Milan.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni