STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 11 Juni 2015

FLOYD "MONEY" MAYWEATHER ANEDELEA KUWABURUZA WANAMICHEZO KWA MKWANJA MREFU.

BONDIA mahiri Floyd Mayweather ndio mwanamichezo anayelipwa zaidi katika kipindi cha miezi 12 iliyopita kea mujibu wa jarida ya Forbes. 

Orodha ya wanamichezo wanaolipwa zaidi inamuonyesha Mayweather ambaye pia aliongoza orodha hiyo mwaka jana, akiwa amekusanya dola milioni 300. 

Pesa nyingi kati hizo amezipata katika pambano lake na Manny Pacquiao ambaye naye ameingiza dola 160 zinazomfanya kukaa katika nafasi ya pili. 

Nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo yuko katika nafasi ya tatu kea kujikusanyia dola milioni 79.6 akifuatiwa na Lionel Messi katika nafasi ya nne aliyekusanya dola milioni 73.8. 

Nafasi ya tano inashikiliwa na nyota wa tenisi Roger Federer aliyekusanya dola milioni 67, akifuatiwa na nyota wa mpira wa kikapu LeBron James aliyekusanya dola milioni 64.8 huku nyota mwingine wa kikapu Kevin Durant yeye akikusanya dola milioni 54.1. 

Wengine ni nyota wa mchezo wa gofu Phil Mickelson aliyejikusanyia dola milioni 50.8 akifuatiwa na Tiger Woods dola milioni 50.6 na kumi ya orodha hizo inafungwa na nyota mwingine wa kikapu Kobe Bryant aliyekusanya dola milioni 49.5.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox