Leo hii ndio siku ambayo sakata la Ramadhan Singano a.k.a Messi lilikua linasikilizwa kwenye ofisi za TFF ambapo pande mbili zilikutana chini ya TFF.
Baada ya kikao kirefu muafaka uliofikiwa chini ya TFF ni kwamba kuvunjwa kwa mikataba yote miwili ambayo inatofautiana. kikao kimeamua kwamba mkataba wa alionao Messi uvunjwe na mkataba walionao Simba uvunjwe waingie makubaliano mapya
Upande wa Singano haujakubaliana na maamuzi hayo kwasababu unamtaka yeye akubaliane na Simba tena. Lakini kwa mujibu wake ni kwamba anatakiwa kuwa huru kama mkataba umevunjwa na sio kukubaliana upya na Simba. Singano anataka kuwa mchezaji huru ndio aamue mwenyewe kama kuongea na Simba au club nyingine.
Kama TFF wamewataka Singano na Simba kuzungumza upya kwasababu
mikataba yote imefutwa, maana yake wakishindwana, Singano anachukua hamsini
zake na sio lazima akubali kuendelea kuichezea Simba.
Wakati huo huo, mtandao huu umefahamishwa kuwa, Katibu mkuu
wa TFF, Mwesigwa amemuandikia barua Singano ambayo nakala yake amechukua
mwenyekiti wa SPUTANZA, Bwana Kisoky ikithibitisha
maamuzi yaliyochukuliwa na kuwa ushidi
wa maazimio ya kikao hicho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni