STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Ijumaa, 5 Juni 2015

JUVENTUS YASAJILI MKALI WA MABAO MUARGENTINA



         JUVENTUS YASAJILI MKALI WA MABAO MUARGENTINA
 
KLABU ya Juventus imekamilisha usajili wa mshambuliaji Murgentina, Paulo Dybala kutoka Palermo kwa dau la Pauni Milioni 24. 
 
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 alikuwa anahusishwa na kuhamia Chelsea, Manchester United na Arsenal baada ya kuwa msimu mzuri Italia, ambako amefunga mabao 13 katika mechi 35 za Ligi.
 
Lakini amechagua kubaki Italia na amesaini Mkataba wa miaka mitano na 'KIbibi Kizee' cha Turin, kwa sababu walionyesha dhamira haswa ya kumsajili na kuamua kuipotezea Ligi Kuu ya England. 


  tovuti ya klabu hiyo imesema: "Juventus Football Club inaweza kutangaza kufikia makubaliano na Palermo juu ya huduma za Paulo Dybala, ambaye amesaini Mkataba wa miaka mitano.
 
Akizungumza baada ya uhamisho huo, Dybala alisema kwamba: "Juventus ni klabu ambayo ilikuwa inanihitaji mimi zaidi. "Walifanya jitihada za dhati kunisajili na ndiyo maana nimefanya uamuzi,".

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox