STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 11 Juni 2015

KOMBE LA DUNIA LA WANAWAKE LIMEVUNJA YA REKODI YA KUTAZAMWA NA WATU WENGI.

WARATIBU wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA wamedai kuwa michuano ya Kombe la Dunia la wanawake inayoendelea katika miji sita nchini Canada imeshavunja rekodi ya kutazamwa na idadi kubwa ya watu. 

Zaidi ya watu milioni 1.8 kutoka Canada walishudia wenyeji hao wakiifunga China katika siku ya ufunguzi wa michuano hiyo Jumamosi iliyopita. 

Katika taarifa yake FIFA imesema idadi hiyo ya watazamaji wa luninga nchini Canada in kubwa kulinganisha na mechi zingine za michuano hiyo zilizowekwa katika rekodi. 

Nchini China zaidi ya watazamaji milioni 2.3 walishuhudia nchini yao ikipokea kichapo, na kuipita idadi ya watazamaji milioni 1.3 ambayo walishuhudia nchi yao ikiondolewa katika michuanop hiyo katika hatua ya makundi mwaka 2011. 

Marekani wao waliwavutia watazamaji zaidi ya milioni 3.3 wakati wakiichapa Australia mabao 3-1 huku Japan nao ambao ndio mabingwa watetezi wakitazamwa na watu zaidi milioni 4.2 wakati wakicheza na Switzerland. 

Kwa upande wa mchezo wa Uingereza dhidi ya Ufaransa mashabiki wapatao milioni 1.5 walushudiwa mchezao huo kwa Uingereza na idadi kama hiyo pia wakishuhudia nchini Ufaransa huku wageni wa mashindano hayo Uholanzi wakipata watazamaji milioni moja wakati wakicheza na New Zealand.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox