STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Ijumaa, 5 Juni 2015

MAVUGO KUTUA MSIMBAZI


                     MAVUGO KUTUA MSIMBAZI


 SIMBA SC imekaribia kabisa kukamilisha usajili wa mchezaji mpya wa sita kuelekea msimu ujao, na huyo si mwingine bali mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Laudit Mavugo.
 
Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Simba SC, Collins Frisch yuko mjini Bujumbura kukamilisha usajili wa mchezaji huyo na habari zisizo rasmi zinasema, amefanikiwa.
 
Chanzo cha habari kutoka Simba SC kimedai kwamba Mavugo tayari ni mchezaji wa Wekundu wa Msimbazi kwa miaka miwili ijayo.
 
Kijana huyo aliyezaliwa Oktoba 10, mwaka 1989 kwa sasa anachezea Vital’O ya kwao Burundi, lakini awali alichezea Kiyovu na Polisi za Rwanda na aliyekuwa kocha wa Simba, Mserbia Goran Kopunovic ndiye aliyempendekeza mkali huyo wa mabao asajiliwe.
 
Kopunovic amewahi kufanya kazi na Mavugo katika timu ya Polisi ya Rwanda, kabla ya wawili hao kuihama timu hiyo kwa wakati tofauti.
 
Iwapo Simba SC itamtangaza rasmi Mavugo kuwa mchezaji wao mpya- atakuwa mchezaji wa sita kusajiliwa ndani ya kipindi cha wiki tatu, baada ya awali Wekundu hao wa Msimbazi kuwasaini kipa Abraham Mohammed wa JKU, mabeki Samih Hajji Nuhu wa Azam FC, Mohammed Fakhi wa JKT, kiungo Peter Mwalyanzi wa Mbeya City na mshambuliaji Mussa Hassan Mgosi kutoka Mtibwa Sugar.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox