KIUNGO Lansana Kamara kutoka Sierra Leone amesema anafurahia mazoezi katika klabu ya Yanga na ana imani mabingwa hao wa Tanzania Bara watamsajili kwa ajili ya msimu ujao.
Lansana, ambaye alikuwa akichezea timu ya Umea FC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Sweden, ameiambia Goal, anafurahia mazoezi ya timu hiyo na ushindani ni mkubwa kwake licha ya idadi ndogo ya wachezaji kuhudhuria mazoezi ya timu hiyo.
“Imani yangu ni kucheza Yanga msimu ujao kabla ya kuomba nafasi ya kufanya majaribio nilikutana na kocha mkuu wa Yanga, Hans Pluijm na kufanya naye mazungumzo kuelekea ndoto yake ya kutua katika klabu hiyo.
Timu ya Yanga imeanza mazoezi Jumatatu wiki hii katika uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi kuu Tanzania Bara pamoja na michuano ya kombe la Kagame inayotarajia kuanza mwezi ujao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni