Mshambuliaji wa Mtibwa sugar Ame Ally amefanikiwa kujiunga na Azam Fc baada ya leo kusaini mkataba wa kuitumikia Azam FC.
Kwa mujibu wa mtandao wa Azam FC, mfungaji bora wa Mtibwa sugar msimu uliokwisha Ame Ally amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia Azam FC.
Ame aliyejiunga na Mtibwa sugar msimu uliopita akitokea visiwani Zanzibar aliongoza vyema safu ya ushambuliaji ya mtibwa sugar na kuifanya isikamatike katika michezo 7 ya mwanzo ya ligi huku yeye akiwa ametikisa nyavu mara nne katika michezo hiyo saba ya mwanzo.
Ame anaingia Azam FC kuchukuwa nafasi ya Gaudency Mwaikimba ambaye mkataba wake na Azam FC umekwisha na inasemekana yuko mbioni kujiunga na Majimaji FC ya Songea.
Usajili wa Ame Ally ndio usajili wa kwanza kufanywa na mabingwa hao wa msimu wa 2013/14, na unaongeza ushindani katika nafasi ya ushambuiliaji ambayo ipo chini ya nahodha John Bocco, samba,ba na Didier Kavumbagu, Kipre Tcheche na Joseph Kimwaga
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni