Beki wa Mnigerian, David Faramola Oniya ameanguka ghafla na kufariki dunia uwanjani.
Oniya aliyekuwa anaichezea T Team iliyokuwa ikipiga mechi ya kirafiki dhidi ya Kelantan alianguka na kufariki dunia.
Mnigeria huyo aliyekuwa na miaka 30 alianza mechi hiyo akionekana ni mwenye afya njema kabisa.
Licha ya kukimbizwa hospitali ikiwa ni juhudi za kumuokoa, Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa T-Team, Syahrizan Mohd Zain alisema walielezwa alishapoteza maisha licha ya madaktari kuwa tayari kumsaidia.
DAILY MAIL
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni