STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Ijumaa, 12 Juni 2015

MKURUGENZI WA MAWASILIANO FIFA ATIMULIWA KWA KULETA UTANI.

MKURUGENZI wa mawasiliano wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Walter De Gregorio ametimuliwa baada ya kutoa kauli ya utani kuhusu shirikisho hilo katika luninga huko Uswisi. 

Katika kipindi kimoja maarufu cha mahojiano nchini humo, Gregorio alitania kuwa rais wa FIFA, katibu mkuu na mkurugenzi wa mawasiliano wote wanasafiri katika gari moja ambalo linaendeshwa na polisi. 

Mara baada ya kauli hiyo FIFA ilitoa taarifa baadae kuwa De Gregorio ameamua kujiuzulu wadhifa wake huo lakini wapekuzi wa mambo wanadai kuwa alitimuliwa na rais wa shirikisho hilo Sepp Blatter. 

Blatter mwenyewe mapema mwezi huu alitangaza kujiuzulu pindi utakapofanyika uchaguzi mpya wa nafasi yake hiyo ikiwa zimepita siku nne toka ateuliwe kuliongoza shirikisho hilo kea muhula wa tano.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox