STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 8 Juni 2015

TAIFA STARS ‘B’ YACHAPWA 2-0 NA RWANDA;


                         

   
                                    TAIFA STARS ‘B’ YACHAPWA 2-0 NA RWANDA;

TIMU ya pili ya taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars B’ leo imefungwa mabao 2-0 na wenyeji Rwanda Uwanja wa Amahoro mjini Kigali katika mchezo wa kirafiki.

Mabao ya Amavubi yamefungwa na Yannick Mukunzi na Patrick Sibomana moja kila kipindi, wakati Rashid Mandawa alikosa bao la wazi, baada ya kugongesha mwamba kufuatia pasi nzuri ya Atupele Green.

Pamoja na kufungwa Taifa Stars B iliyo chini ya kocha Salum Mayanga (pichani juu) ilicheza vizuri, bahati tu haikuwa yao.

Rwanda jana ilicheza na Kenya na kutoka sare ya bila kufungana, wakati mchezo wa utangulizi leo, Kenya imeifunga Sudan Kusini 2-0.

Kikosi cha Stars kilikuwa; Said Mohamed, Hassan Kessy, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Joram Mgeveke, Hassan Isihaka, Simwanza Emmanuel, Mudathir Yahya/Malimi Busungu, Hassan Dilunga/Deus Kaseke, Amri Kiemba, Kelvin Friday/Atupele Green, Rashid Mandawa.

Kikosi cha kwanza cha Taifa Stars kipo kambini Addis Ababa kikijiandaa na mchezo wa kwanza wa kufuzu Fainali za Mataifa Afrika mwaka 2017 dhidi ya Misri wikiendi ijayo mjini Alexandria.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox