VIGOGO wa Misri, Al Ahly na Zamalek wote wamemaliza kileleni mwa makundi baada ya mzunguko wa kwanza Kombe la Shirikisho Afrika mwishoni mwa wiki.
Ushindi wa 2-0 jana wa Zamalek nyumbani dhidi ya AC Leopards Kongo, umewafanya waongoze Kundi B kwa kufikisha pointi tisa, wakati Ahly baada ya kuifunga 1-0 Etoile du Sahel ya Tunisia juzi mjini Alexandria sasa wanaongoza Kundi A kwa kufikisha pointi saba.
Mechi nyingine za mwishoni mwa wiki, CS Sfaxien ya Tunisia ilifungwa 1-0 nyumbani na Orlando Pirates ya Afrika Kusini na Esperance ya Tunisia ilifungwa pia nyumbani 2-1 na Stade Malien ya Mali.
Al Ahly ina pointi saba kileleni mwa Kundi A, ikifuatiwa na ES Sahel yenye pointi sita, Stade Malien pointi nne na Esperance ambayo haina pointi inaburuza mkia.
Zamalek ina ponti tisa kileleni mwa Kundi B, ikifuatiwa na Orlando Pirates pointi sita CS Sfaxien pointi nne na AC Leopards pointi moja.
Mechi za mzunguko wa pili Kombe la Shirikisho zitaanza Agosti 8 mwaka huu, Orlando Pirates wakiikaribisha CS Sfaxien, AC Leopards wakiwakaribisha Zamalek, Stade Malien wakiwa wenyeji wa Esperance na ES Sahel wakiwakaribisha Al Ahly.
MISIMAMO YA MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA
Kundi A
P | W | D | L | GF | GA | GD | Pts | ||
1 | Al Ahly (Misri) | 3 | 2 | 1 | 0 | 4 | 0 | 4 | 7 |
2 | ES Sahel (Tunisia) | 3 | 2 | 0 | 1 | 2 | 1 | 1 | 6 |
3 | Stade Malien (Mali) | 3 | 1 | 1 | 1 | 2 | 2 | 0 | 4 |
4 | Esperance (Tunisia) | 3 | 0 | 0 | 3 | 1 | 6 | -5 | 0 |
Kundi B
P | W | D | L | GF | GA | GD | Pts | ||
1 | Zamalek (Misri) | 3 | 3 | 0 | 0 | 5 | 1 | 4 | 9 |
2 | Orlando Pirates | 3 | 2 | 0 | 1 | 3 | 2 | 1 | 6 |
3 | CS Sfaxien (Tunisia) | 3 | 0 | 1 | 2 | 1 | 3 | -2 | 1 |
4 | AC Leopards (Kongo) | 3 | 0 | 1 | 2 | 1 | 4 | -3 | 1 |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni