Nahodha mwandamizi wa Machampions wa England, Chelsea, John Terry leo ame-make Headline kwenye vyombo vya habari.
Terry
ameweka wazi kwamba ana nia ya kuichezea Chelsea angalau kwa miaka
miwili ijayo na amesisitiza kwamba hatafuata nyayo za magwiji wenzake Petr Cech na Frank Lampard ambao kwa nyakati tofauti wameamua kuzichezea timu nyingine za Barclays Premier League.
Msimu
uliopita, Lampard aliichezea kwa mkopo Manchester City kutokea New York
City ya Marekani, wakati Cech amejiunga na Arsenal majira haya ya
kiangazi.
Terry, 34, ambaye amekuwa na Chelsea tangu akiwa mtoto amesema ataendelea kuwepo England na anatarajia kustaafia soka Stamford Bridge.
"Kama Chelsea wanaamua kuniachia sitakuwa na la kufanya, lakini nadhani nitaendelea kucheza, ila sio timu ya Premier League"
"Kufikia Chrismas nitakuwa na miaka 35, nadhani naweza kucheza miaka mingine tena".
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni