Simba kupitia msemaji wake Hajji
Manara amesema, imepokea taarifa kutoka klabu ya Bidvest Wits FC ya
Afrika Kusini alikokwenda Jonas Mkude kufanya majaribio ikisema kwamba,
wamemuona mchezaji huyo katika majaribio na wameridhika na majaribio
yake.
Afisa habari wa klabu ya Simba
Hajji Manara amesema wamepokea barua kutoka klabu ya Bidvest Wits FC
ikieleza wameridhishwa na kiwango alichokionesha Mkude na kuahidi kuwa
wataendelea kumfatilia huku (Tanzania) aliko ili kuendelea kujua
maendeleo yake.
Jonas
Mkude amefanya majaribio, na kwa mujibu wa klabu ile ni kwamba, klabu
imetutumia barua kutupa taarifa kuwa imeridhishwa na kiwango chake na
wataendelea kumfuatilia huku alipo kwasababu wao walimchukua kwasababu
ya ‘trial’ na majibu yake ndio hayo”, amesema Manara.
Majuma kadhaa yaliyopita kiungo
wa Simba Jonas Mkude alielekea nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kufanya
majaribio kwenye klabu ya Bidvest Wits ambayo inashiriki ligi kuu ya
nchini humo (PSL) lakini haukupita muda mrefu Mkude akarejea jijini Dar
es Salaam na badae kujiunga na kikosi cha Simba kilichopo Lushoto
kujiandaa na msimu ujao wa ligi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni