Chelsea
wamefanikiwa kuibuka na ushindi dhidi ya PSG baada ya kufanikiwa
kushinda kwa changamoto ya mikwaju ya penati 6-5, katika mchezo wa
kuwania 'International Champions Cup' uliopigwa usiku wa kuamkia leo
katika dimba la Bank of America Stadium.
Chelsea wamerudi kwa kasi baada ya hapo awali kupokea kipigo cha mabao 4-2 kutoka kwa New York Red Bulls siku ya Jumatano.
Zlatan
Ibrahimovic ndiye alikuwa wa kwanza kuona lango la Chelsea baada ya
kufunga bao zuri katika dakika ya 25, kabla ya Victor Moses
kuisawazishia Chelsea goli mnamo dakika ya 65.
Katika changamoto za mikwaju ta Penati Courtois ndio aliibuka shujaa baada ya kuifungia Chelsea penati nzuri kabisa ya ushindi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni