Baada ya kombe la dunia 1938 kufanyika mipango ikawa ni
maandalizi ya kombe la dunia 1942 lakini kutokana na vita vya dunia
vya pili kombe la dunia halikuweza kuchezwa vilevile 1946
halikufanyika 1950 Brazil wakapewa uwenyeji baada ya hali ya mambo kuwa tulivu Duniani.
Fainal zikawa timu zote za amerika ya kusini wenyeji Brazil dhidi ya Uruguay
ndani ya dimba la Maracana-Rio de Janeiro ambalo
lilikuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji 199,854.
Mtanange
uliteka hisia kubwa huku wa brazil wakiwa na imani kubwa kutwaa ubingwa huo
walifurika ndani ya maracana takribani mashabiki 205,000 wakahudhuria mchezo huo ambapo wingi huo ni rekodi lakin pia ulipitiliza
idadi iliyotakiwa ktk uwanja ya mashabiki 199,854.
Mwamuzi akiwa ni George Reader
wa Uingereza mnamo dakika ya 47 Brazil
wakawa wa kwanza kufunga kupitia Albino Friaca Cardoso winga wa Sao Paulo wakati huo, lakini dakika ya 66 Juan Alberto Schiaffino Villano wa Uruguay akasawazisha.
Dakika ya 79 Alcides Edgardo Ghiggia akaipatia Uruguay goli la pili na la ushindi na kuwaacha
wabrazil wakiduwaa kwa kushindwa kuchukua kombe la dunia ndani ya dimba la
nyumbani.
Hiko ndicho tulizungumza kwenye sports details siku ya jana kwenye kumbukumbu za michuano hiyo Taarifa kutoka nchini Uruguay zinasema Alcides Edgardo Ghiggia mchezaji pekee aliebakia hai katika kikosi kilicho cheza 1950 amefariki Dunia akiwa na miaka 88 wakati ambao Uruguay inakumbuka miaka 65 tangu awatoe kimasomaso katika dimba la Maracana nchini Brazil.
Ukiachilia mbali tukio hilo la kukumbukwa pia wanamichezo wengi watamkumbuka kwa kauli yake kuwa " ni binadamu watatu tu waliofanikiwa kuunyamazisha uwanja wa Maracana ni yeye mwenyewe, Papa na mwanamuziki Frank Sinatra.
R.I.P-GHIGGIA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni