MFARANSA
Morgan Schneiderlin amefungua akaunti yake ya mabao mapema tu
Manchester United akiichezea kwa mara ya kwanza kabisa ikishinda 1-0
dhidi ya Club America usiku wa kuamkia leo katika ziara ya kujiandaa na
msimu Marekani.
Kiungo
huyo alifunga bao hilo pekee katika ushindi huo dakika ya tano tu baada
ya kwenda hewani kuifuata krosi ya Juan Mata na kuidondeshea nyavuni.
Schneiderlin, Matteo Darmian na
Memphis Depay wote walicheza dakika zote 45 mjini Seattle, wakati Bastian Schweinsteiger pia aliichezea kwa mara ya kwanza United baada ya Louis van Gaal kubadilisha wachezaji wote 11 walioanza na kuingiza wengine kipindi cha pili.
Adnan
Januzaj na Ander Herrera wote walikaribia kufunga, lakini haikuwa
bahati yao na sasa United inaelekea California kucheza na San Jose
Earthquakes katika mchezo mwingine kwenye ziara hiyo Jumatano.
Kikosi
cha Man United kipindi cha kwanza kilikuwa; Johnstone, Darmian, Jones,
Blind, Shaw, Carrick, Schneiderlin, Young, Mata, Memphis na Rooney
(Nahodha).
Kipindi
cha pili: Lindegaard, McNair, Smalling (Nahodha), Evans, Blackett,
Lingard, Schweinsteiger, Herrera, Pereira, Januzaj na Wilson.
Club
America: Club America: Gonzalez, Mares/Andrade dk46, Aguilar/Marin
dk68, Sambueza (Nahodha), Goltz, Arroyo/Rivera dk68, Samudio/Colula
dk68, Guemez/Guerrero dk68, Quintero/Diaz dk68, Martinez/Sanchez dk68 na
Buron.
Mechi zijazo ziara ya Man United ni
Julai 22,San Jose Earthquakes [ Uwanja wa Avaya,California]
Julai 25 Barcelona [Uwanja wa Levi,California]
July 30 Paris Saint-Germain (Uwanja wa Soldier Field, Illinois)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni