STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatano, 8 Julai 2015

KAULI YA MESSI BAADA YA KUVUNJWA KWA MKATABA WAKE NA SIMBA









Winga wa zamani wa klabu ya Simba Ramadhani Singano ‘Messi’ amesema kwa sasa anahitaji muda wa kutulia na familia yake kabla hajajua ni wapi ataelekea kwa ajili ya kuendelea kucheza soka, jana kamati ya sheria, maadili na hadhi za wachezaji chini ya mwenyekiti wake Richard Sinamtwa iliuvunja mkataba kati ya Simba na mchezaji huyo kufuatia klabu ya Simba kutofuata masharti ya vipengele vya mkataba wao.

Messi amesema mpaka sasahivi bado hajajua ni wapi ataelekea kwani muda mwingi alikuwa anafikiria suala lakela mkataba kati yake na klabu yake ya zamani (Simba SC).
“Napenda kumshukuru mwenyezi Mungu kwa matokeo yaliyotolewa na TFF na kamati yake kwa ujumla lakini paia sina budi kuwashukuru waandishi wa habari kwa kunisapoti tena sana na pale nilipokosea naomba mnisamehe”, Messi alisema.

“Kikubwa nilikuwa nasubiri suala langu hili la kimkataba na Simba liishe maana akili yangu yote ilikuwa inafikilia suala hili na nilikua sifikilii suala jingine lolote.  Sijajua nitaelekea wapi maana muda wa usajili bado upo, bado nataka nikae na familia yangu niwasikilize baba zangu, kaka zangu na washauri wangu, kwahiyo mpaka muda huu bado sijajua chochote”, aliongeza.

“Mimi siwezi kuusemea moyo wa mtu lakini mimi bado nawakumbuka (Simba) tena sana na nimeshasahau kwa yote yale ambayo tumefanyiana kwa mazuri na mabaya na naomba pia kama kuna ubaya wowote ambao nimeufanya basi wanisamehe ten asana”, Messi aliomba radhi.


Maamuzi ya kuuvunja mkataba yaliyofanywa jana na kamati ya sheria , maadili na hadhi za wachezaji yanamfanya Messi kuwa mchezaji huru na anaweza kusajiliwa na klabu yoyote ile ambayo atakubaliana nayo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox