Mchezaji
huyo wa kimataifa wa England anataka kulazimisha dili la kutimka
Anfield na anaelewa kabisa akibaki England ataweza kufanikisha dili hilo
kwa urahisi zaidi kuliko kama atasafiri na timu kwenda kwenye ziara
Mashariki ya Mbali pamoja na Australia.
Manchester
City wanatarajia kuipelekea Liverpool ofa nyingine ya tatu kwa ajili ya
kumnasa kinda huyo mwenye miaka 20 huku Liverpool ikiwa imeshakataa
pauni 35 ambayo ilikuwa ni ofa ya kwanza kutoka Man City, haikuishia
hapo City ikaongeza na kupeleka ofa ya pili ya pauni 40 ambayo pia
ilikataliwa wakati wao Liverpool wanataka walipwe pauni milioni 50 kama
ada ya uhamisho wa mchezaji huyo.
Sterling
ambaye Jumatatu aliripoti Melwood (uwanja wa mazoezi wa Liverpool) kwa
ajili ya mazoezi ya kujiandaa na msimu ujao, anatarajiwa kuungana na
kikosi cha Brendan Rodgers kitakacho safiri kuelekea Thailand siku ya
Jumapili.
Mechi yao ya kwanza wakiwa ziarani itakuwa Bangkok Jumanne ijayo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni