Baada
ya kamati ya sheria, maadili na hadhi za wachezaji ya shirikisho la
soka Tanzania (TFF) chini ya mwenyekiti wake Richard Sinamtwa kutoa
maamuzi wa kumtangaza mchezaji Ramadhani Singano ‘Messi’ kuwa yupo huru
na anaweza kusajiliwa na klabu yoyote anayoitaka, uongozi wa iliyokuwa
klabu yake (Simba) kupitia mwenyekiti wake wa usajili Zacharia Hans
Poppe umetoa kauli juu ya uamuzi huo.
“Mimi
binafsi nimelishughulia hili suala lakini nimesikitishwa sana na haya
maamuzi na sikutegemea watu wa kwenye ile kamati hasa mwenyekiti kama
wangefikia maamuzi kama yale.
Kwasababu nilimchukulia mwenyekiti yule
kama mtu mmoja mwenye kufuata haki, lakini leo sita sita kusema amekuwa
‘very bias’ na sijui amebadilika vipi kwasababu limezungumzwa na leo
ilikuwa ni mara ya pili tu lakini tulishalizungumza huko nyuma na
alilielewa vizuri”, amesema Poppe.
“Mambo
yote tuliyoyazungumza kule nyuma anakuja kuyabadilisha leo kwasababu
hataki kukubali kuwa tumemlipa pesa laki sita za mkataba wa nyumba ambao
unataka tumlipe kwa miaka mitatu na bado mkataba haujaisha, sijui hata
nisemeje, sikutegemea watu wa sampuli kama ile, kaliba kama ile wanaweza
kutoa maamuzi kama yale”, ameeleza.
“Kipengele
hakisemi tutampa nyumba, kipengele kinasema tutamlipa laki sita katika
kipindi chake cha ‘contract’ ambacho ni miaka mitatu. Laki sita ya
‘accommodation’ kwa kipindi chote cha mkataba wake.
Tulichotakiwa sisi
ni kuthibitisha ni kwamba je, laki sita hiyo kapata? Lakini imeenda
mbali zaidi hata kama hajapata mkataba wake bado haujaisha. Nafasi ya
kulipa hiyo laki sita ipo na ‘hatuja-default’ chochote lakini cha ajabu
ndio hicho”, alizidi kufafanua.
“Sisi
hatuna cha kufanya maana kikao hicho kina ‘power’ na kikishafanya
maamuzi hakuna namna ambayo unaweza kuyapinga wala namna ambayo unaweza
kukatia rufaa katika vikao vyetu vya hapa. Neno lao ni la mwisho na watu
wakitoa maamuzi ya vile basi inabidi yatekelezwe labda kama unataka
kwenda CAF sasa hayo ni mambo ya kamati ya utendaji”, aliongeza.
“Mimi
binafsi ningependa kulifatilia hili suala mpaka mwisho wake kwasababu
nikitazama matukio ya huko nyuma maamuzi mbalimbali yamechukuliwa dhidi
ya Simba halafu yanaishia hivi katikati halafu lawama zinakuja kwa
Simba.
Tukiangalia kwenye ule uamuzi wa Yondani ambapo tulipeleka
mikataba miwili wakwetu na wale wengine walikuja na mkataba mwingine
yalitoka maamuzi ya ajabu ya namna hiyohiyo sasa maamuzi ya namna hii
yanatuumiza”, alimaliza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni