Mshambuliaji
wa kimataifa wa Tanzania anaekipiga kwenye klabu ya TP Mazembe ya Congo
Mbwana Samatta amedhihirisha kwamba anataka kucheza soka barani Ulaya
baada ya kuikataa ofa ya miamba ya soka la Afrika timu ya Zamalek ya
Misri ambao walikuwa wakimtaka lakini nyota huyo amesema mtazamo wake
kwa sasa ni kucheza soka Ulaya.
Meneja
wa mchezaji huyo Jamal Kisongo amethibitisha kupokea ofa kutka klabu ya
Zamalekh wakitaka kumsajili mchezaji wake Mbwana Samatta lakini wao
hawako tayari kumwachia mchezaji huyo aendelee kucheza soka barani
Afrika na badala yake wanataka akacheze barani Ulaya.
“Maombi
hayo yalikuwepo lakini sisi tulikataa kwasababu tuliona ni vyema kama
ataenda nje ya Afrika na yeye mwenyewe (Samatta) hakuwa tayari kwenda
kucheza huko ingawa walikuwa wamefika pesa nzuri tu kutaka kuwalipa
Mazembe”, amesema Kisongo.
“Kuna
timu nyingi sana za Ulaya zinazomtaka lakini Katumbi hataki aondoke
mpaka amalize michuano ya vilabu bingwa imalizike, sisi tunasubiri
michuano hiyo imalizike na baadae anaweza kuondoka kama mchezaji huru
maana mkataba wake unaelekea ukingoni”, ameongeza.
Mkataba
wa Samatta na TP Mazembe unamalizika Aprili 2016 lakini ikifika mwezi
Oktoba mwaka huu, na hapo atakuwa huru kufanya mazungumzo binafsi na
klabu yoyote ambayo itaonesha nia ya kuhitaji huduma yake.
Samatta
alipata fursa ya kwenda kufanya majaribio kwenye klabu ya CSKA Moscow
ya Urusi lakini alipata majeraha wakati akiendelea na majaribio hivyo
kushindwa kumaliza muda wa majaribio uliokuwa umepangwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni